Saturday, 26 April 2014

Evil sex sehemu ya kwanza "simulizi iliyojaa visaa vingi vya mapenzi maijini na binaadamu mtafaruku katika mapenzi"


                                                         
EVIL SEX   (1)  

Kikundi cha wanafunzi wapatao kumi na tano wa chuo kikuu wakibishana juu ya uwepo wa majini katika dunia

"Mimi nabishana hadi asubuhi hakuna majini duniani"

"Eddy wewe tatizo lako mbishi mimi nakuambia majini wapo duniani"

"Unajua ni nini,nyinyi waoga mimi siwezi kuamini mashetani hapa duniani"

Mjadala ukanyamaza gafla baada ya gari aina ya Range rover kusimama na kushuka wasichana watatu weupe warefu wenye kila mvuto katika macho ya mwanaume wakiwa na mabegi ya mgongon

"Jamani vyombo hivyo"

"Eddy watoto waibukie"

"Si muende nyinyi mimi ndio mumeniona malaya"

Wasichana wakapita mbele ya kundi la wavulana na kuwasalimi wengine wakaitikia isipo kuwa Eddy akabaki akiwatazama hadi wanazamia kwenye ngazi za gorofa

"Oya mcheki Eddy anavyo wakodolea mimacho hao madem"

"Mmm jamani macho hayana pazia"

Taratibu Eddy akanza kupandisha ngazi na kuwaacha wezake wakimtania kwa maneno ya utani,Eddy akaanza kuchungulia darasa moja baada ya jingine kuwatafuta wale wasìchana

Akajikuta amefika darasa la mwisho la gorofa na kuwakuta wale wasichana wakiwa na wasichana wengine,Kutokana darasa si lake akajikuta akizuga kwa kuweka earphone masikioni na kusikiliza mziki utokao kwenye simu yake

Eddy akajikuta amekaa zaidi ya lisaa zima pasipo wanafunzi kuruhusiwa na profesor wao,Baada ya muda wakaruhusiwa wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengne

"Sory sister"

"Bila samahani kaka"

"Naitwa Eddy nipo mwaka wa kwanza nasomea maswala ya accounts"

"Nashukuru kukufahamu.Unajingine?"
"Ndio nahitaji kukutoa chakula cha usiku"

"Ok niachie namba yako"

Eddy akampa namba ya simu huku akiachia tabasamu pana

"Ooohoo nimesahau dada unaitwa nani?"

"Nitakuambia baadaye"

Eddy akabaki anathaminisha umbo la yule msichana kwa nyuma akastuka akiguswa kwa nyuma

ITAENDELEA...............


Writter:Ahmedy

No comments:

Post a Comment