Pata mautamu mbali mbali kupitia blog hii ya Mautamu Nyang'anyang'aaa ya TZ & nje za Nchi
Saturday, 26 April 2014
EVIL SEX SEHEMU YA TANO (5) NI SIMULIZI YA KUSISIMUA HISIA ZAKO SOMA HAPA KWA UNDANI ZAID UBURUDIKE....
EVIL SEX SEHEMU YA TANO (5)
Mlio mkali wanaousikia Janet na Maria ukaambatana na matone matone ya mvua na kuwafanya Janet na Maria kukimbilia kwenye moja la jengo linalotumika kuhifadhia vitabu visivyo tumika
Mvua ikazidi kunyesha ikiambatana na radi kali pamoja na upepo na ikawalazimu Janet na Maria kuingia ndani huku taa zikiwa zimezimwa
"Maria tujibanze humu haka kamvua kapite kwanza"
"Na hili giza mwenzio sina imani kabisa humu ndani"
"Mungu atasaidia wangu"
***
Dareen akaendelea kuinyonya shingo ya Eddy na kusababisha Eddy kupungukiwa na nguvu za mwili
Dareen akajilaza pembeni mwa Eddy ambaye hajielewi,Baada ya masaa mawili Eddy akarudi katika hali yake ya kawaida akamtazama Dareen ambaye anakoroma fofofo
Taratibu Eddy akazishika nguo na taratibu akaanza kuzivaa kwa tahadhari kubwa bila Dareen kustukia kitendo hicho,hakuona haja ya kuva shati taratibu akanyata kuelekea mlangoni
"Eddy unakwenda wapi?"
Sauti ya uchovu ya Dareen ilisikika vizuri na kusababisha Eddy kustuka ambaye amekaribia kufikia kitasa cha mlango huku akiwa ameshika shati lake mkononi
"Mmm na....na...kw...enda h...ap...o chin..i"
Eddy alipata kigugumizi cha gafla na kumfanya Dareen kuachia tabasamu kisha akasimama na kumfwata Eddy alipo na kumshika mkono
"Njoo Eddy wangu mbona unataka kunikimbia mmmm...?"
Eddy akajikuta hana cha kuzungumza,Dareen akamshika Eddy mkono na kuuzungusha kiunoni mwake na kuanza kukichezea kifua cha Eddy
"Eddy sasa upo sawa na mimi humezi kubadilika tena"
"Kivipi?"
"Utaelewa tu mpenzi"
Eddy akajikuta anajishika eneo la shingoni na kuhisi maumivu
"Umenifanya nini hapa shingoni?"
Eddy alizungumza kwa jazba huku akimtaza Dareen kwa hasira
"Eddy huwezi kunifanya kitu chochote mimi na wewe ni familia moja"
Kauli za Dareen zikazidi kumchanganya Eddy na kumshukuma Dareen pembeni kisha akafungua mlango na kutoka
Eddy akajikuta ana tazamana na Dareen ambaye aliachana naye chumbani huku akiwa na nguo nyeusi juu hadi chini,Woga ukaanza kumtawala Eddy akajaribu kukimbi ila Dareen akamzuia kwa mkono mmoja huku akimshik kifuani
"Eddy huwezi kunikimbia hapa duniani"
***
Janet na Maria wakaanza kusikia milio ya vitabu vikipigwa ukutani kwa woga wakakimbilia katika mlango walio ingilia wakastukia ukijifunga kwa nguvu na wakajikuta wakigeuka nyuma kutazama ni nani anaye angusha vitabu na kuona kivuli kikubwa kikiwafwata walipo
ITAENDELEA..............ENDELEA KUFUATILIA ZAID KWENYE HII BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment