Sunday, 27 April 2014

EVIL SEX SEHEMU YA TISA (9)



                                EVIL SEX SEHEMU YA TISA (9)


Janet akabaki anatazamana na Dareen huku akikosa cha kuzungumza

"Eddy tutazungumza kesho"

Janet akaondoka na kuwaacha Eddy na Dareen wakicheka

Machozi yakaanza kumlenga lenga Janet hadi akajikuta akigongana na Jimy

"Shem vipi mbona unalia?"

"Mmmm.."

"Janet tena afadhali nimekuona"

"Jimy sijisikii vizuri naomba uniache kwa sasa"

"Janet hichi ninacho kuambia ni muhimu sana juu ya kunusuru mapenzi yenu"

Janet akakaa kimya na kumsikiliza Jimy

"Kuna hali ambayo imempata Eddy ambayo kusema kweli hata mimi inaniogopesha Eddy sio mtu bali ni jini"

"Nini..?"

Janet alionekana kustuka

"Mimi kwa macho yangu nilimshuhudia Eddy akitoa machozi meusi huku macho yake yakiwa yamebadilika"

"Weee Jimy hembu acha masihara Eddy huyu wangu hawezi kuwa kama unavyosema"

"Wewe si unamuona Eddy alivyo siku hizi hakujali wala hana muda na wewe tena kama umemchunguza kwenye shingo ana alama ya kung'atwa"

"Sasa tutafanyaje?"

"Mimi nitawasaidia"

Sauti ya kike ikasikika ikiwaambia na kuwalazimu wageuke na kumtazama ni nani aliyezungumza.Wakakutana na msichana ambaye ni mara yake ya kwanza kumuona

"Naamini munajiuliza mimi ni nani na nimejuaje kitu munacho zungumza"

"Samahani dada hii mada haikuhusu wewe fanya tu upite"

Janet alizungumza huku akimtazama msichana wa watu

"Janet hembu ngoja tumsikilize labda ana chamana cha kutuambia.."

"Tumsikilize nini wakati hawa ndio waibaji wa waume za watu hapa chuo"

"Dada usimzarau usiye mjua kwani hujui nani atakaye kusaidi katika matatizo yako"

"Ni hivi Eddy ambaye ni mpenzi wako kwa sasa ana hali ambayo si binadamu japo mwili ni wakibinamu"

Alizungumza huku akimtazama Janet machoni

"Naomba munifwate"

***

"Eddy naomba nika kutambulishe kwetu"

Dareen alizungumza huku akimtazama Eddy machoni mwake

"Kwenu?"

"Ndio kwani nataka ukapajue kwetu kwenye asili yangu ambayo wewe pia unayo"

"Unaonaje tukaenda nikimaliza masomo?"

"Mimi nahitaji leo"

"Mmmm mbona umenistukiza sana"

"Hapana huwa sisi hatupendi kutoa ahadi kwa mtu alafu ishtimie"

"Mimi sipo tayari kwa hilo swala"

ITAENDELEA..........................................

No comments:

Post a Comment