Saturday, 26 April 2014

Hadi nao wanafanya michepuko na binaadamu fuatilia simulizii kali sana ya( EVIL SEX SEHEMU YA TATU) soma kwa undani zaid



                                           EVIL SEX SEHEMU YA TATU (3)



Eddy kwa furaha akakumbatiana na rafiki yake kisha akakaa kiti cha pembeni yake

"Eddy sory kwa kukusumbua"

"Hakuna tatizo vipi nikuagizie chakula gani?"

"Eddy huko nilipotoka nimekula nimeona nijeshushie na huu mvinyo"

Muhudumu akaja kumuhudumia Eddy kisha akaondoka

"Ehee nimekumbuka hivi uliniambia utaniambia jina lako"

"Mimi naitwa Dareen"

"Waoo unajina zuri"

"Mbona kawaida wangu"

Eddy na Dareen wakaendelea kunywa na kula mpaka wakalewa

"Eddy baby siwezi kurudi nyumbani nataka tulale pamoja"

"Kweli baby?"

"Ndio"

Eddy akanyanyuka na kwenda mapokezi kuchukua chumba akarudi alipo Dareen wakaelekea chumbani
***

Janet usiku mzima hakupata usingizi kila mara moyo wake ukawa unastuka,taratibu akaamka na kuchukua biblia yake na kusoma baadhi ya mistari kisha akapiga magoti na kusali

Joto kali likazidi kutawala katika chumba alicholala akili yake ikaanza kumuwaza Eddy mpaka akakatisha maombi

"Maria Maria Maria"

Janet akamuamsha Maria ambaye anakoroma

"Mmmm.."

"Amka unipeleke kwa Eddy ninahisia mbaya juu yake"

"Saa ngapi saa hizi?"

"Saa sita usiku"

"Mmm Janet bwana wewe huoni muda umekwenda?"

"Maria nakuomba tu mpenzi nisaidie kwenye hili"

Taratibu Maria akajinyanyua huku akipiga miyayo ya usingizi akavb nguo wakatoka pamoja

Wakiwa njiani upepo mkali ukaanza kuvuma mpaka wakaanza kujikunyata

Wakahisi kitu kikipiti nyuma yao wakageuka haraka hawakuona kitu

"Janet umesikia hicho kitu?"

"Ndio sijui ni nini?"

Upepo ukazidi kuvuma majani ya miti ikazidi kupeperushwa

Wakaanza kusikia vishindo vikija nyuma yao kwa mwendo wa taratibu

Maria akamkumbatia Janet ambaye akaanza kusali taratibu kimoyo moyo

Mlio mkali wa mtoto mchanga ukasikika ukilia mbele yao jambo lililozidi kuwaogopesha

"Janet mimi nilikuambia tusije huku umeona sasa"

Janet hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kumuomba Mungu wake huku akizidi kuelekea mbele kwenye hostel za wavulana
~~
Eddy akaanza kumvua nguo Dareen moja baada ya nyingine huku akiwa ana mthaminisha

ITAENDELEA.............................

No comments:

Post a Comment